Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Edward Lowassa
Akizungumza katika mkutano wa Baraza la wanawake la CHADEMA, iliyakutanisha makundi mbalimbali ya wanawake nchini wenye mahitaji mbalimbali Mhe.Lowasa amesema nia ni kumjengea uwezo mwanamke wa kujikwamua kiuchumi.
Mhe.Lowasa amesema wanawake wana kero nyingi zinazowakabili ikiwa ni pamoja na huduma duni za afya ya uzazi,umbali wa kupata maji safi na salama ,kuwa na vipato duni licha ya kushiriki katika ujasiria mali hivyo anaomba apewe ridhaa ya kuwaongoza ili awasadie kuondokana na kero hizo.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa BAWACHA Bi. Grace Tendega amesema wanawake bado wanakabiliwa na changamoto nyingi hususani katika sekta ya afya ambapo vifo vya wakati wa kujifungua na vya watoto chini ya miaka mitano vimeongezeka.