Friday , 6th Nov , 2015

Mkurugenzi wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini LHRC Dkt. Hellen Kijo-Bisimba amekemea tabia ya uvunjwaji wa demokrasia uliotumiwa na vyombo vya usalama kuendelea kushikilia vifaa vyao walivyokuwa wanafanyia kazi ya uangalizi wa uchaguzi

Mkurugenzi wa kituo cha haki za binadamu nchini LHRC Dkt.Hellen Kijo-Bisimba

Dkt. Bisimba amesema kuwa vyombo hivyo wamekuwa wakivifanyia kazi kwa mujibu wa sheria na vibali vyote vyakufanya hivyo lakini wanashangaa jeshi la polisi kuendelea kuvishikilia.

Dkt. Kijo-Bisimba ameyasema hayo leo jijini Dar es salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa ni lazima sasa jeshi la polisi nchini lifanye kazi zake kwa kufuata katiba ya nchi na democrasia pindi wafanyapo kazi zao na waache kufanya kazi kwa kusukumwa na vyama vya siasa.

Bisimba amesema kuwa hata kukamatwa kwa vifaa vyao kunaonekana dhahiri kuwa kuna msukumo wa kisiasa nyuma yake kwa sababu hata askari hao wanaoshikilia vifaa hivyo wakiulizwa kuhusiana na kwanini wamekamata vifaa vyao hawana jibu la kutosha.