Thursday , 24th Apr , 2014

Chama cha sheria cha watetezi wa mazingira nchini Tanzania LEAT kimetaka kufanyike kwa mapitio ya sera za mazingira na mali asili ili kuwa na mfumo mzuri wa kudhibiti vitendo vya ujangili na uwindaji haramu.

Mkurugenzi wa LEAT Mwanasheria Dk Rugemeleza Nshala amesema hayo leo na akafafanua kuwa ubovu wa sera na sheria umesababisha baadhi ya watendaji kujihusisha na uwindaji haramu.

Nshala ameonya kuwa hazina ya wanyamapori nchini huenda ikatoweka kabisa iwapo hatua za makusudi za kudhibiti vitendo vya ujangili na uwindaji haramu hazitachukuliwa.

Tags: