Josee Ntabahungu, Meneja wa Programu ya Kuendeleza Wanawake katika Shirika la Care International, Burundi
Kikao cha 60 cha Kamisheni kuhusu hali ya Wanawake (CSW60) kikiendelea hapa kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa, serikali na sekta binafsi zimeshauriwa ziwasaidie wanawake kwa kuwawezesha kifedha.
Meneja wa Programu ya Kuendeleza Wanawake katika Shirika la Care International, nchini Burundi, Josee Ntabahungu, amekiambia kikao cha jopo la ngazi ya juu kwamba kuna haja ya ushirikiano katika uratibu na uwekezaji katika miradi ya wanawake ili kuwawezesha wanawake kifedha.
Amesema kufanya hivyo kutachangia maendeleo siyo tu katika maisha ya wanawake hao binafsi, lakini pia katika jamii na nchi kwa ujumla.
Amesema mwanamke akisaidiwa watoto wanaweza kwenda shule bila matatizo yoyote uchumi na maendeleo ya nchi yanakuawa hivyo ameshauri wadau waweze kuwasaidia wanawake kwa wingi zaidi ili kukuza uchumi kwa haraka