Kaleb Gamaya - Katibu Mkuu TLS
Katibu Mkuu wa Chama cha Wanasheria cha Tanganyika Law Society (TLS) upande wa Tanzania Bara Bw. Kaleb Gamaya amesema ni muhimu kwa kila mwananchi kutambua kuwa kutafuta suluhisho katika ofisi za watendaji na kwa viongozi wa kisiasa si suluhisho la changamoto zao bali wajenge tabia ya kuwashirikisha wanasheria kabla ya kuingia makubaliano yoyote.
Naye Mwenyekiti Kamati ya Msaada wa kisheria kutoka chama hicho Bi. Maria Matui amesema msaada wa kisheria ni haki za binadamu na kwamba ili maendeleo endelevu yafikiwe kikamilifu ni wajibu wa serikali na jamii kwa ujumla kuhakikisha kuwa wanafuata sheria ili kutowanyima haki watu wengine.
Wakiongelea muswada wa sheria ya msaada wa kisheria ambao unajadiliwa hivi sasa, wameiomba serikali kupunguza masharti kwa wasaidizi wa kisheria hasa katika kipengele kinachomzuia msaidizi kutojihusisha na siasa kwani kuna wanasheria wengine ambao ni wabunge hivyo kipengele hicho kinaleta mkanganyiko juu ya utekelezaji wake.






