Monday , 3rd Aug , 2015

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Feruzy Bano ametangaza matokeo ya kura za maoni Jimbo la Arusha Mjini mapema jana, nakusema kwa sasa hawezi kusema aliyeshinda kwa kura ndio mshindi, sababu bado wana vikao vya kuchunja na atakayerudishwa jina lake.

Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM, Feruzy Bano.

Amewataja wagombea na kura zao kuwa ni Philemon Monaban (5320) akifuatiwa na Justin Nyari (1894), Moses Mwizarubi (1005), Reuben Mwiteni (171), Thomas Munisi (832),Victor Njau (752), Emmanuel Ole Njoro (90),Mohammed Omary (171), Swalehe Kiluvia (446), Hamisi Migire (305), Weraufoo Munisi (832) na Mustafa Panju (498).

Baada ya kumaliza kuwatangaza wagombea hao na kura zao, alizuia watu kushngilia sana kwa madai kuwa kuna vikao vya uteuzi vinaendelea.

Hata hivyo wakati wakitangaza matokeo hayo wagombea waliokuwepo watatu ambao ni Philemon Monaban, Justin Nyari na Mustafa Panju na wengine wote hawakuwepo kwa madai kuwa wamechakachuliwa kura zao na hawajaridhika na matokeo.

Naye Wera ufoo Musnia, amesema kama yeye alikosewa picha zake zilitolewa nyeusi kama mjaluo, wakati yeye mweupe na mzuri, hivyo ni sababu ya kukosa kura maana wapiga kura wengi wanaangalia picha.

Mgombea Victor Njau, amesema yeye alikuwa na asilimia kubwa ya ushindi, ila kura zake zimeibiwa sana na mashabiki wa Philemon Monaban na hali hiyo haitakaa kuleta ukombozi wa kweli Tanzania.

Kwa upande wa washindi Philemon Monaban na Justin Nyari wameshukuru kwa kura walizopata na kusema wanasubiri haki zaidi itatendekea vikao vya juu.