Katibu tawala wa mkoa wa Njombe, Gidion Mwinami
Kauli hiyo imetolewa na wataalam wa kudhibiti maambukizi ya virusi vya UKIMWI mkoani Njombe, katika kikao cha Tathimini ya mapambano ya UKIMWI mkoani humo.
Akifungua mkutano huo Kaimu Katibu tawala wa mkoa wa Njombe, Gidion Mwinami alisema kuwa kumekuwa na baadhi ya wanawake maeneo ya kuuza vinywaji licha ya kufanya kazi hiyo lakini huwa wanafanya kazi nyingine majira ya jioni.
Ameongeza kuwa kutokana na kuwepo kwa mzinguko huo wataalamu na taasisi zisizo za kiserikali (NGO's) zihakikishe kuwa zinapambana na changamoto za aina hiyo na kuhakikisha kuwa muingiliano huo hauongezi maambukizo.
Wilfred Mkungilwa ni Meneja wa shilika la PSI mkoa wa Njombe na Abubakari Magege ni mratibu wa UKIMWI mkoa wa Njombe TACAIDS wanasema kuwa kumekuwa na changamoto ya 'madada poa' wanao hamahama na kutumiwa kama chambo huku wengine wakitafuta pesa.
Magege ameongeza kuwa katika mfumo huo wa kuwahamisha unachangia sana maambukizi ya VVU.