Monday , 29th Aug , 2016

Shirikisha la Viwango Tanzania (TBS) limekifungua kiwanda cha kuzalisha mabati cha Quansheng International Trading, cha jijini Dar es Salaam kwa kuzalisha mabati bila ya kuwa leseni ya ubora.

Kiwanda cha Mabati

Akizungumza muda mfupi baada ya kukifunga kiwanda hicho Mkaguzi wa Ubora wa Bidhaa kutoka TBS, Yona Afrika, amesema kiwanda hicho kilikuwa kikizalisha kiholela mabati ya kuezekea na kuyaingiza sokoni Kinyemela.

Afrika amesema ni kosa kwa mzalishaji wa bidhaa yoyote au huduma kuingiza kwenye soko lolote ndani na nje ya Tanzania bila kuthibitisha ubora wake kwa kuwa hali hiyo inaweza kuleta madhara kwa watumiaji na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake mwakilishi wa kiwanda hicho alikiri kuwa wamekuwa wakiendesha biashara hiyo ya mabati kwa kuzalisha na kuuza bila leseni ya ubora ya TBS kwa sababu walishaanza mchakato wa kuitafuta.