Saturday , 20th Jun , 2015

Chama cha Mapinduzi CCM kimeahidi kutatua mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wadogo wa kata ya Nyarugusu mkoani Geita na shirika la madini la taifa STAMICO na kampuni tanzu ya kutoka nchini Marekani ya Tanzam 2000,

Sehemu ya eneo la Nyarugusu

Chama cha Mapinduzi CCM kimeahidi kutatua mgogoro baina ya wachimbaji wadogo wadogo wa kata ya Nyarugusu mkoani Geita na shirika la madini la taifa STAMICO na kampuni tanzu ya kutoka nchini Marekani ya Tanzam 2000, kwa kumiliki eneo kubwa la uchimbaji madini huku wananchi wakikosa maeneo ya uchimbaji.

Hatua hiyo ya CCM inafuatia kilio cha wananchi hao, kilichowasilishwa na mbunge wa jimbo la busanda Lolensia Bukwimba na diwani wa kata ya Nyarugusu Ahmad Mbaraka, waliomuomba katibu mkuu kuingilia kati na kutatua kigugumizi cha wizara ya nishati na madini,kupitia shirika la madini la taifa STAMICO, kwa kushindwa kugawa eneo hilo licha ya ahadi ya mheshimiwa Rais ya kuiagiza wizara na STAMICO kuwapatia wachimbaji wadogo eneo la kuchimba madini.

Akihutubia maelfu ya wakazi wa mji wa Katoro mkoani Geita,katibu mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana,amewataka radhi wananchi hao kwa niaba ya serikali ya chama cha mapinduzi,kwa kuwa na kigugumizi katika kutatua mgogoro huo wa muda mrefu,na kuwaomba kuwa na imani naye,juu ya uzoefu wa utatuzi wa migogoro baina ya serikali na wananchi.

Kinana ameahidi kurejea na kuwapa majibu ya uhakika kama watapewa au la kupitia mkutano wa hadhara kwenye mji wa Katoro STAMICO wameingia ubia na kampuni tanzu ya kimarekani ya Tanzam 2000 ikiwa na hisa asilimia 45 na STAMICO wakimiliki hisa asilimia 55