Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro amesema kuwa kilimo cha tumbaku nchini Tanzania kimekosa tija ikilinganishwa na nchi jirani za Malawi na Zimbabwe, kutokana na uwajibikaji duni wa baadhi ya maafisa ugani wanaozolotesha uzalishaji.
Mkuu huyo wa mkoa amesema hayo wakati akiogea na wakulima wa tumbaku wilayani Chunya,
amesema Chunya inazalisha nusu tani kwa ekari moja wakati nchi jiarani zinalisha takriban tani mbili kwa ekari, na kwamba zao hilo likizalisha vizuri linaweza kusaidia maendeleo na upatikanaji wa ajila kwa wananchi
Meneja wa chama kikuu cha wakulima wa tumbaku chunya Bakari Kasia amesema katika msimu wa mwaka 2013 na 2014 wanatarajia kuzalisha tumbaku yenye thamani ya zaidi ya dola mil. 38 ingawa baadhi ya wakulima wamesema kuwa licha ya kuhamasika na kilimo hicho na kuzalisha kwa wingi lakini wanakata tamaa kutokana na kuyumba kwa soko.
Katika wilaya ya Chunya zao la tumbaku linaingiza zaidi sh. Bil. 45, na ni zao pekee linalo saidia kwa asilimia kubwa katika mapato ya halimashauri ya wilaya ya Chunya.