
Aliyewahi kuwa waziri mkuu wa Tanzania, hayati Edward Moringe Sokoine (kulia) akiwa na rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Julius Kambarage Nyerere.
Mkuu wa mkoa wa Arusha Magesa Mulongo amesema maandalizi ya maadhimisho hayo yamekamilika na kuwataja baadhi ya viongozi watakaoshiriki kuwa ni pamoja na rais wa awamu ya tatu Benjamini Mkapa, mjane wa baba wa taifa mama Maria Nyerere watendaji mbali mbali wa serikali na wananchi kwa ujumla.
Bw. Mulongo amesema katika maadhimisho hayo shughuli mbalimbali zitafanyika kwa lengo la kumuenzi kiongozi huyo shujaa aliyepigania wanyonge katika kipindi chote cha maisha yake na kwamba makundi mbali mbali yamejitokeza kushiriki, na wanatarajiwa kufikisha ujumbe unaolenga kuenzi na kuendeleza yote aliyoyaanzisha hayati Edward Moringe Sokoine aliyefariki mwaka 1984 kwa ajali ya gari