
Akiongea na EATV leo katika ofisi za jumuiya hiyo Jijini Dar es salaam, Gulam ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga amesema, benki ya NMB ilitoa kiasi hicho cha pesa kwa jumuiya hiyo kwaajili ya ufadhili wa Tuzo ya Meya (Mayor Awards) na kwamba Katibu huyo huyo hakuwasilisha kiasi chote na badala yake aliwasilisha shilingi milioni 60 huku kiasi cha shilingi milioni 90 kikiwa hakijulikani kilipo.
Mukadam amesema, uamuzi wa kumsimamisha uliamuliwa na kamati tendaji ya ALAT Taifa na mkutano mkuu wa ALAT taifa, ambapo iliundwa tume ndogo kuchunguza upotevu wa kiasi hicho cha pesa na kuamuliwa kuwa apishe uchunguzi dhidi yake kwa upotevu wa pesa hizo.
Gulam Mkadam
Aidha Mstahiki Mukadam amesema, uchunguzi dhidi yake utafanywa na CAG na kwamba pesa hizo hazikuwekwa kwenye akaunt ya ALAT na badala yake zilihifadhiwa kwenye akaunti binafsi ijulikanayo kama 'Vision Investment'.