Thursday , 24th Jul , 2014

Kesi ya mauaji ya mtoto nasrah mvungi inayowakabili washtakiwa watatu imeingia katika hatua nyingine baada ya jalada la kesi hiyo kupelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Marehem mtoto Nasra enzi za uhai wake akiwa na baba yake

Kesi ya mauaji ya mtoto nasrah mvungi inayowakabili washtakiwa watatu imeingia katika hatua nyingine baada ya jalada la kesi hiyo kupelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali.

Washtakiwa hao kwa mara nyingine tena wamepandishwa kizimbani, mbele ya hakimu wa mahakama ya hakimu mkazi mkoa wa Morogoro, Mary Moyo, ambapo mwendesha mashtaka wa polisi Aminatha Mazengo ameiambia mahakama kuwa, jalada la kesi hiyo limepelekwa kwa mwanasheria mkuu wa serikali, hivyo kuiomba mahakama kupanga tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa kwa kesi hiyo.
Hakimu Moyo ameridhia ombi hilo la upande wa mashtaka, na kupanga Agosti 6 mwaka huu kesi hiyo ifikishwe tena mahakamani hapo kwaajili ya kutajwa, kwani mahakama hiyo haina mamlaka kisheria kusikiliza kesi ya mauaji na washtakiwa hao wamerudishwa rumande kutokana na kesi hiyo ya mauaji kutokuwa na dhamana.

Washtakiwa hao awali walikuwa wakikabiliwa na shtaka la kula njama na kufanya vitendo vya ukatili dhidi ya mtoto Nasrah Mvungi kabla ya baadaye mashtaka yao kubadilishwa na kuwa ya mauaji baada ya mtoto aliyedaiwa kufanyiwa ukatili, Nasra Mvungi, kufariki dunia wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya taifa ya muhimbili alikokuwa amelazwa.