
Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema mkoani Geita, Alphonce Mawazo enzi za uhai wake.
Mapingamizi hayo yalikuwa ni pamoja na kwamba, mtoa maombi katika kesi ya madai namba 10 ya mwaka 2015 Bw. Charles Lugiko ambaye ni baba mdogo wa marehemu Alphonce Mawazo hana uhalali wa kisheria kuwasilisha maombi hayo kwa vile yeye si baba mzazi wa marehemu.
Akitoa maamuzi katika kesi ya awali jana Jaji Lameck Mlacha, alisema mlalamikaji Lugiko ana haki ya msingi kama baba mdogo wa marehemu Mawazo kwa mila za kusimamia msiba wa mtoto wa kaka yake.
Mahakama imekubaliana na hoja za mawakili za mtoa maombi na kuamua kuruhusu kesi ya msingi kufunguliwa.
Akizungumza na waandishi wa habari nje ya Mahakama hiyo wakili wa mlalamikaji John Malya na kuelezea hatua zaidi zinazofuata na kuwa kesi hiyo itaanza kusikilizwa leo chini ya hati ya dharura.
Mawazo aliuawa Novemba 14, mwaka huu na watu wasiojulikana katika kijiji cha Katoro Geita kwa kupigwa na vitu vyenye ncha kali mwilini.