Friday , 15th Jan , 2016

Rais Uhuru Kenyatta amesema majeshi ya Kenya yatawinda wapiganaji walioshambulia kambi ya majeshi ya Umoja wa Afrika nchini Somalia na kuua wanajeshi.

Rais Kenyatta amethibitisha kwamba kambi ya wanajeshi wa Muungano wa Afrika (Amisom) katika eneo ambalo linasimamiwa na majeshi ya Kenya ilishambuliwa asubuhi.

“Tutawawinda wahalifu waliohusika katika matukio ya leo. Damu ya wanajeshi wetu haikumwagwa bure,” amesema kupitia taarifa kwa vyombo vya habari.

Wapiganaji wa Al-Shabab wamesema waliua wanajeshi wengi wa Kenya baada ya kuvamia kambi ya majeshi ya AU Somalia.

Kundi hilo limesema liliiteka na kudhibiti kambi hiyo mjini el-Ade na kuua wanajeshi 63 wa Kenya.

CHANZO BBC