Tuesday , 21st Jul , 2015

Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF, awamu ya tatu wilayani Karatu mkoani Manyara ametenga kiasi cha sh. milioni 247.6 katika mpango wake wa ugawaji wa fedha ili kunusuru kaya masikini 5,736 wilani humo.

Mkurugenzi wa Miradi wa TASAF Bw. Amadeus Kamagenge akielezea manufaa ya mpango unaotoa fursa ya ajira kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini PSSN.

Mratibu wa Tasaf wilayani Karatu, Resteli Hayuma amesema ugawaji fedha hizo Halmashauri ya karatu imepata kiasi cha shilingi milioni 247.6 kwa ajili ya Kaya hizo.

Hayuma amesema lengo la mpango huo ni kuzisaidia Kaya masikini na zilizoko katika mazingira hatarishi kwa kuwapatia walengwa ruzuku kuwa kuwawezesha kupata mahitaji ya msingi kama shule, huduma za elimu na afya.

Amesema pamoja na huduma hizo pia wanalenga kuinua hali ya maisha na kuongeza kipato katika familia hizo angalau kila mtanzania aweze kupata milo mitatu kwa siku na kuwajengea uwezo wa kuwekeza.