
vinavyoendelea kuongezeka ili kunusuru vizazi vijavyo.
Akizungumza na maelfu ya waumini wa kanisa hilo katika uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mtume katika eneo la Moshono Jijini Arusha Askofu amesema ili kuthibiti ongezeko la ukiukwaji wa haki za watoto pamoja na kupambana na vitendo viovu vya ulawiti kwa watoto wadogo jamii inapaswa kuchukua nafasi yao kuwalinda watoto.
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Yakobo Mtume Padre Cyril Imohiosen amesema viongozi wa dini wana nafasi kubwa katika kutoa mafundisho kwa waumini ili kuhakikisha matendo maovu yanakomeshwa ndani ya jamii huku akiwataka waumini kuonyesha ushirikiano katika shughuli za maendeleo.
Waumini wa Kanisa hilo wamewapongeza viongozi wa dini wanaopaza sauti zao kupinga ukatili unaofanywa na baadhi ya watu kwa watoto wadogo huku wakiziomba mamlaka husika kuchukua hatua za kisheria ili kudhibiti vitendo hivyo.