Monday , 24th Aug , 2015

Rais Mstaafu wa Bunge la Africa na Mbunge wa Zamani wa Jimbo la Ukerewe Mh. Getrude Mongela amesema kampeni za vijembe na mipasho hazina tija kwa taifa ambapo hali hiyo inaweza kuvuruga amani.

Balozi Gertrude Ibengwe Mongela

Mh. ameongea hayo leo katika kipindi cha Supermix cha East Africa Radio amesema kuwa kutokua na sera kunafanya wanasiasa wengine watumie lugha sizizo na staha hivyo kushauri wanasiasa watumie lugha za staha katika kufanya kampeni ili kudumisha amani.

Amesema kuwa vyama vinatakiwa kutengeneza ilani ambayo itaweza kueleweka kwa wananchi na kupunguza muda wa kutumia lugha chafu na badala yake waweze kueleza sera za chama chao.

Aidha amevitaka vyombo vya habari kutumia kalamu zao vizuri ili kufikisha ujumbe kwa wananchi na kutaka vyombo vya hivyo viepuka kununulia pamoja na kutanguliza maslahi ya kibiashara zaidi na kupelekea kuingia nchi katika hatari ya machafuko.

Akitolea mfano wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda ya mwaka 1994 yalichochewa na vyombo vya habari ambavyo vilipekea machafuko hayo na kuongeza kuwa Tanzania inahitaji kujiepusha na hali hiyo.