Kamishna wa maadili ya utumishi wa umma Jaji mstaafu Salome Kaganda
Jaji Kaganda ameyasema hayo wakati wa kuapishwa kwa maofisa 58 wa jeshi la polisi ambao waliteuliwa na Rais Dkt. John Magufuli hivi karibuni na kuwataka kuhakikisha wanatimiza wajibu wao sehemu ya kazi ili Jeshi liwe mfano wa kuigwa.
''Ni vyema mkaanzisha kamati za maadili katika jeshi la polisi kwa kuwa siku hizi malalamiko yanatoka kwa askari wa chini yenu, na wengine wanalalamikia hata IGP sasa kungekuwa na kamati za maadili mambo yenu mngeweza kuyamaliza huko huko'' Amesema Jaji Mstaafu Kaganda.
''Ninyi mmeaminiwa na Rais wajibu wenu kahakikisheni maadili na nidhamu kwa waliyo chini yenu yanaimarika na muache kuwakatisha tamaa walio chini yenu, kwa mfano unakuta kuna askari amekamata muhalifu ila baada ya muda mfupi anaachiwa kutokana na kujuana na mkubwa jambo hili ni baya na mnawakatisha tamaa watu wa chini yenu'' Amesisitiza Jaji Kaganda
Kwa mujibu wa IGP Ernest Mangu Jumla ya maofisa waliopandishwa vyeo ni maafisa 25 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) na kuwa Naibu Kamishna wa Polisi (DCP). Na 34 kutoka cheo cha Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP) na kuwa Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) ambapo wawili hawakuweza kufika kwa kuwa mafunzoni nje ya nchi.
Aidha IGP amesema mchuano wa kuwapata ulikuwa ni mkali kwa kuangalia utendaji wao wa kazi katika maeneo yao ya kazi.







