Jumla ya watoto 66 wamezaliwa usiku wa jana kuamkia Sikukuu ya Krismasi katika hospitali za Amana, Temeke na Mwananyamala za Jijini Dar es Salaam huku hospitali ya Amana ikikumbwa na changamato ya kupokea wajawazito wengi zaidi.
Akizungumza na East Africa Radio leo Afisa Muuguzi Kiongozi wa hospitali ya Amana Ilala, Florensia Ndumbaro amesema kuwa katika hospitali hiyo watoto 33 wamezaliwa kati ya hao watoto wa kiume ni 18 na wa kike ni 15 na kuongeza kuwa changamoto kubwa ni wajawazito wengi wanaokwenda hospitali hiyo ni kutoka wilaya zingine.
Kwa upande wa Hospitali ya Temeke watoto 12 wamezaliwa wa kiume wakiwa 4 na wakike ni 8 ambapo waliojifungua kwa upasuaji ni wawili, na katika hospitali ya Mwananyamala watoto waliozaliwa ni 21 wa kike 12 na wakiume 4 na waliozaliwa kwa upasuaji ni wa 5.