Wednesday , 10th Sep , 2014

Kikao cha Rais wa Jamhuri wa Muungano Tanzania na kituo cha Demokrasia Tanzania TCD kimefikia muafaka na kukubaliana Bunge maalum la katiba liishie October 4 Mwaka huu na kumalizia mchakato huo baada ya Uchaguzi mkuu mwakani.

Mwenyekiti wa Kituo cha Demokrasia John Momose Cheyo.

Akizungumza baada ya kikao hicho Mwenyekiti wa TCD, Mh. John Cheyo amesema kuwa hatua hiyo pia imetokana na kubainika kuwa muda uliopo kwa sasa hautoshi kuweza kukamilisha katiba itakayotumika kwa ajili ya uchaguzi mwakani.

Cheyo amesema hatua itakayofata baada ya kupendekezwa kwa katiba hiyo ni kura ya maoni ambayo ilitakiwa kufanyika April mwakani itasitishwa na kusogezwa mbele na kuendelea mbele baada ya uchaguzi mkuu October.

Katika hatua Nyingine Cheyo amesema pia wamekubaliana matayarisho kwa ajili ya uchaguzi wa vijiji,vitongoji na mitaa yaanze haraka iwezekanavyo kwa serikali kuchukua hatua za kisheria ili uchaguzi ufanyike mapema mwakani.