Thursday , 1st Oct , 2015

Rais Jakaya Kikwete amewataka wabunge wa bunge la Marekani kufunga masoko ya pembe za ndovu na faru duniani kama njia yenye uhakika wa kukomesha ujangili dhidi ya wanyamapori katika nchi za Afrika.

Rais Kikwete akihutubia Kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Mjini New York ambapo katika hotuba hiyo alielezea masuala mbalimbali

Rais Kikwete amewataka wabunge hao kizisaidia nchi za Afrika kifedha ili kukomesha ujangili huo kwa sababu wabunge hao tayari wameshaitangazia dunia kuwa wanazo fedha za kutosha kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya ujangili.

Akizungumza mjini New York, Marekani mbele ya baadhi ya marais wenzake wa nchi za Afrika wanaokabiliana na ujangili Rais Kikwete amesema kama kweli wabunge wa Marekani wakiamua kutumia nguvu za taifa lao kufunga masoko ya meno ya ndovu, pembe za faru basi tatizo hilo litakwisha.

Rais Kikwete amesema wapingaji wa ujangili duniani wameandaa dola bilioni 13.2 za kufanya kazi ya kukabiliana na ujangili duniani lakini fedha hizo hazionekani katika nchi za Kiafrika.