Dkt. Kikwete ameyasema hayo leo alipotembelea maonesho ya 40 ya kimataifa ya biashara ya jijini Dar es salaam maarufu kama sabasaba na kueleza kuwa bidhaa nyingi zilizoandaliwa katika maonesho ya mwaka huu zinaubora wa hali ya juu hivyo nivyema bidhaa hizo zikapewa kipaumbele na kuwafikia walaji ili kuwapa faida wajasiriamali.
Aidha Dkt. Kikwete amepongeza bidhaa zilizotokana na tafiti mbalimbali yakiwemo mazao na mbegu zilizofanywa na chuo kikuu cha Dar es Salaam kuwa ni vyema zikatumiwa na wazalishaji wa mazao ili kuweza kuwasaidia wakulima katika uzalishaji wa mazao yenye tija kwaajili ya biashara na chakula.
Dkt Kikwete amesema, UDSM kama chuo kimeweza kufanya nafasi yake hasa katika sekta ya utafiti jukumu lililobaki ni la tafiti hizo kutumiwa na walengwa katika kuendeleza uzalishaji wa mazao.


