Tuesday , 12th Apr , 2016

Shirika moja lisilo la kiserikali la kutoka nchini Japan limeandaa shindano la wazo la kibunifu la kibiashara kwa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo vijana kutoka nchini Tanzania.

Shirika moja lisilo la kiserikali la kutoka nchini Japan limeandaa shindano la wazo la kibunifu la kibiashara kwa makundi mbalimbali ya kijamii wakiwemo vijana kutoka nchini Tanzania ambapo moja ya lengo la shindano hilo ni kukuza na kusaidia wajasiriamali wa Tanzania.

Meneja wa Maendeleo ya kibiashara kutoka shirika hilo Bw. Allex Kapungu amesema shindano hilo litafanyika katika nchi tano za Afrika na pia lina lenga kulijenga wazo hilo bunifu kuwa biashara halisi.

Miongoni mwa nchi zitakazo shiriki ni pamoja na Tanzania, Kenya, Rwanda, Zambia na Zimbabwe huku mshindi wa shindano hilo atapata fursa ya kutembelea nchi ya Japan kuona fursa mbalimbali za kiuchumi zinazopatikana huko.