Friday , 15th May , 2015

Serikali imewataka wazazi na walezi kushirikiana pamoja katika malezi ya familia ili kutokomeza ukatili wa kijinsia ambao huwakumba zaidi wanawake, watoto na watu wenye ulemavu.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sofia Simba

Wito huo ulitolewa jana na Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sofia Simba wakati akizindua siku ya kimataifa ya familia ambayo inafanyika leo, ambapo pia alizindua zana za mawasiliano kuhusu elimu ya malezi kwa familia mjini hapa.

Simba alisema kuwa inasikitisha kuona kuwa kufikia karne hii bado ukatili dhidi ya wanawake, watoto na watu wenye ulemavu unaendelea kushika kasi kwenye baadhi ya maendeleo hapa nchini.

Kwa upande wake Katibu wa Wizara hiyo, Anna Maembe aliwasihi wazazi na walezi hasa wanaume kuwajibika kikamilifu kwa kushirikiana na akina mama katika malezi bora ya watoto wao.

“Tunatambua kuwa katika taratibu za maisha ya jamii zetu wanaume wana nafasi kubwa katika kuleta mabadiliko hivyo wana wajibu mkubwa sana katika kutokomeza ukatili wa kifamilia.” Alisema Maembe.