Waumini wakiwa katika Msikiti wa Ghadafi Mkoani Dodoma (Picha na Maktaba).
Wito huo umetolewa na Imam wa msikiti wa Sunni Muslim Jamaat Nunge, Sheikh Ahmed Zubeir, wakati wa swala ya Iddi el Fitri iliyoswaliwa katika viwanja vya Jamhuri Mjini Dodoma ikiwa ni kuashiria kumalizika kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Sheikh Zubeir amesema waislam na jamii kwa ujumla inapaswa kutendeana mema wao kwa wao pamoja na serikali ili kutoa nafasi ya kufanya maendeleo yanahitajika katika jamii kwa kutenda haki na usawa.
Kwa upande wake Mtoa hutuba katika swala hiyo ya Iddi el Fitri iliyoswalia katika viwanja hivyo Ustadh Omari Salum, amewataka waislam wenye uwezo kuwakumbuka watu wanaoishi katika mazingira magumu na masikini wakiwemo mayatima.
Katika Msikiti Mkuu wa Ghadafi Mjini Dodoma, ambao Imam wake ni Kaimu Sheikh Mkuu wa Dodoma Sheikh Ahmed Said, amewaasa waislam kuutunza umoja na amani iliyo nchini lakini akilitaka Jeshi la Polisi Usalama barabarabani kusimamia ipasavyo sheria ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.