Rais wa mahakama ya Afrika Jaji Agustino Ramadhani
Jaji Agustino ameyasema hayo katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Makao makuu ya mahakama ya Afrika jijini Arusha, ambapo pamoja na mambo mengine washiriki walijadili Protokali ya Maputo katika kulinda haki za binaadamu.
Wakiongea katika maadhimisho hayo baadhi ya wanasheria wamesema baadhi ya sheria zinakinzana katika utowaji wa maamuzi kunakochangiwa na sheria nyingi kushindwa kukidhi mahitaji ya wakati husika .
Maadhimisho hayo yamefanyika leo ikiwa pia ni miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mahakama ya Afrika.