Wednesday , 9th Mar , 2016

Ripoti iliyotolewa na Shirika la Kazi Duniani-ILO imesema itachukua karibu miongo saba hadi wanawake watakapopata kipato sawa na wanaume, kama pengo la malipo litaendelea katika kasi ya sasa.

Mwanamke akiwa katika moja ya harakati za kujitafutia Kipato kwa biashara ndogondogo

Shirika hilo limesema kwa sasa wanawake wanapata asilimia 23 chini ya wastani kuliko wanavyopata wanaume, huku asilimia 72 ya wanaume duniani kote wakiwa wameajiriwa na kiwango cha wanawake ni asiliamia 46.

ILO imesema hali hiyo inatokana na ukweli kwamba wanawake wamekuwa wakiutumia zaidi muda wao kufanya kazi za nyumbani na kuwaangalia watoto.

Kiasi ya wanawake wazee milioni 200 duniani kote wanaishi bila kupata pensheni yao, ikilinganishwa na wanaume milioni 115.
Siku ya Wanawake Duniani huadhimishwa Machi 8 ya kila mwaka.