Friday , 25th Sep , 2015

Idadi kubwa ya wanawake wa vijijini hawafikiwi na pembejeo za kilimo na huduma ya ugani licha ya kuchangia asilimia 43 ya nguvu kazi katika kilimo na uzalishaji mali mashambani.

Mkurugenzi wa mradi wa ubunifu katika usawa wa kijinsia na kuimarisha uhakika wa chakula ngazi ya kaya Bi. Rose Kingamkono.

Mkurugenzi wa mradi wa ubunifu katika usawa wa kijinsia na kuimarisha uhakika wa chakula ngazi ya kaya Bi. Rose Kinga mkono amesema hayo mjini Mafinga kwenye semina ya uongozi na upatikanaji wa pembejeo za kilimo na elimu ya ugani wa mwanamke.

Amesema kukosekana kwa huduma hizo kumechangia umasikini kwa wanawake kutokana na kutotambuliwa kama wakulima kwasababu wanawake hawapatiwi fursa ya kumiliki ardhi ambayo ndiyo msingi maendeleo.

Akifungua semina hiyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mufindi Saada Malunde amesema katika msimu ujao wa kilimo halmashauri hiyo itatoa kipaumbele kuhakikisha wanawake wanapata pembejeo za kilimo na huduma ya ugani ili kuongeza tija na uhakika wa chakula ngazi ya kaya.