
Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbulu Hudson Kamoga
Afisa Utumishi huyo anadaiwa kutoa takribani shilingi milioni 21 kwaajili ya mishahara, ambayo ilikuwa inalipwa kutoka 2010, hivyo anatakiwa apatikane ili aweze kuwajibika kisheria katika ubadhilifu huo alioufanya.
Hayo ameyazungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la kujadili na kujibu hoja za mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali , ambapo amebainisha kuwa hoja nyingi zinaonekana ni za muda mrefu, kwasababu watumishi wengi waliifanya halmashauri hiyo kama shamba la bibi la kuja kujichumia fedha.
Hata hivyo Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Hudson Kamoga amesema kuwa, pamoja na hoja hiyo ya nyuma ya wizi wa fedha hizo, lakini watajitahidi kuhakikisha hati yao inazidi kuwa safi.
Baada ya kuhamishwa kwa Afisa Utumishi huyo, ndipo ikajulikana kuwa kuna mishahara hewa inatolewa kwa watumishi hewa kutoka mwaka 2010 hadi 2017.