
Akizungumzia upungufu huo mapema leo hospitalini hapo wakati akipokea msaada wa shuka nyeupe 100 na blanketi 30 kutoka kwa Kanisa la Calvary Temple la Kilombero mjini Arusha, Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk. Josiah Mlay, amesema upungufu ni mkubwa wa vitu hivyo ikizingatiwa kuwa wagonjwa wanakwenda kipindi cha baridi kali.
Amesema mengi kati ya mashuka na blanketi waliyonazo kwa sasa yamechakaa kutokana na kemikali wanazotumia kufulia wakati zinapochafuka wodini, hivyo wanahitaji shuka na blanketi nyingine haraka kabla ya msimu wa baridi haujaanza.
Ametaja mahitaji mengine hospitalini hapo kuwa pamoja na vifaa vya maabara ambavyo kwa sasa ni vichache, hivyo wanaomba msaada kwa wasamaria wema na sio kuiachia serikali ambayo ina majukumu mengi.