Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Mhe. Angella Kairuki
Kairuki ameyasema hayo ikiwa ni moja ya mafunzo kwa wakurugenzi ambao waliteuliwa hivi karibuni na kuapishwa hii leo ikulu jijini Dar es salaam,
Waziri Kairuki amewaaasa wakurugenzi hao kuepuka vitendo vya rushwa na mashinikizo yasitofuata sheria kutoka juu yao ambayo baadaye yataweza kuwaletea shida.
''Hatutakubali Rais atiwe doa kutokana na uzembe wa Mkurugenzi wa halmashauri yoyote , ofisi yangu ipo wazi wakati wowote kama kuna jambo mtahitaji usaidizi, msifanye mambo mkiwa na wasiwasi'' Amesema Waziri Kairuki.
Aidha Waziri amewataadharisha wakurugenzi hao kwamba waepuke rushwa kwani TAKUKURU wapo kazini kila kona ya nchi, pia namba zake zimesambaa nchi nzima hivyo hivyo wasione kama wapo wenyewe katika utendaji.
Pia amewataka Wakurugenzi hao kushirikiana na viongozi wengine katika kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi na kuhakikisha wanatatua kero za wananchi pia kutenga siku za kusikiliza kero za wananchi.

