Moja kati ya Majengo yanayopatika Mji Mkongwe Visiwani Zanzibar ambavyo ni Vivutio vya Utalii.
Mji Mkongwe ambao ni Kivutio cha utalii katika visiwa vya Zanzibar hivyo uliwekwa katika orodha ya maeneo yaliyo hatarini kuondolewa kwenye orodha ya urithi wa dunia.
Katibu Mtendaji wa Tume ya Taifa ya UNESCO nchini Tanzania Dk Moshi Kimizi amesema baada ya majadiliano ya muda mrefu jopo hilo sasa litakutana na pande husika ambazo ni serikali na mamlaka ya UNESCO akisema mjadala utahusu usitishwaji wa majengo ambayo tayari yalikuwa yameanza kujengwa katika maeneo hayo.
Dkt, Kimizi amesema lengo ni kukaa kuelewana na shirika hilo ili kusitisha ujenzi wa mahoteli hayo ili na kusema kuwa wanaamini wataelewana na shrika hilo ili Wazanzibar waweze kufaidika na maliasili zao za Utalii.
UNESCO wamesema kuwa mji huo wa kitalii upo hatarini kotoweka baada ya kuanza kwa ujenzi holela wa majumba katika eneo hilo na pia mabadiliko ya tabia kiasi ya kwamba kutishia uwepo wa eneo hilo kwa muongo mmoja mbele.
Hata hivyo Dk Kimizi amesema ana matumaini kuwa muafaka utafikiwa ili kulinda hadhi ya mji huo muhimu kwa historia ya Afrika Mashariki.