
Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe,na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam, Dkt Vincent Mashinji amesema majaji wanawasiliana na mawakili wa pande zote mbili na kesho kesi hiyo itaanza kusikilizwa.
“Tunashukuru mahakama kwa kutenda haki, na jinsi walivyolichukulia suala la mwenyekiti kwa dharula yake na tumeambiwa tukutane kesho saa mbili asubuhi kwa ajili ya kusikiliza rufaa ya mwenyekiti wetu Mbowe,” amesema Mashinji.
Novemba 23 mwaka huu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Jijini Dar es salaam ilimfutia dhamana Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini, Ester Matiko baada ya kujiridhisha juu ya viongozi hao kukiuka masharti ya dhamana.
Uamuzi huo wa mahakama ulitolewa na Hakimu Mkazi, Wilbard Mashauri wakati kesi ya vigogo saba wa CHADEMA ikisikilizwa, Ester Matiko na Mbowe walikuwa wakituhumiwa kutumia vibaya kibali cha dhamana yao baada kushindwa kuhudhuria kufika mahakamani zaidi ya mara moja bila ya kuomba ruhusa ya mahakama.