Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe.
Mkuu wa mkoa wa Morogoro Dkt. Rajab Rutengwe ametaka maeneo hayo kutengwa ili wafanyabiashara wapate maeneo rasmi ya kufanyia biashara zao na kupunguza au kuondoa kabisa hali ya uchafu na hatari ya maambukizi ya ugonjwa wa kipindupindu na magonjwa mengine yatokanayo na usafi.
Amesema kama mkoa wamekusudia kuwa na wiki ya usafi wa mazingira kuanzia Desemba 2 hadi 9 kwa halmashauri zote kujihusisha na usafi wa mazingira katika maeneo mbalimbali kuanza saa 12 alfajiri hadi saa 2 asubuhi na kuwataka wananchi kufanya usafi kwa mita kumi kutoka kila upande wa makazi wanayoishi.
Maeneo mbalimbali ikiwemo taasisi na watu binafsi na kuzungumza nao kuhusiana na agizo hilo la serikali ambapo afisa uhusiano wa mamlaka ya maji safi na maji taka manispaa ya Morogoro MORUWASA Getrude Salima amesema katika kuteleza agizo hilo la usafi, watajikita pia kufanyia marekebisho maeneo yenye matatizo ya uvujaji wa maji machafu pamoja na kusafisha kisima kikubwa na kuweka dawa huku wananch wakiwa na mawazo tofauti kuhusiana na tamko hilo.