Msemaji wa Jeshi la Polisi , Pierre Nkurikiye, amesema, watu wanne kati yao walifariki eneo la tukio katika shambulizi hilo lililotokea jana Jumapili saa 12:30 jioni katika kijiji cha Shinya.
Bw. Nkurikiye,amesema mtu asiyejulikana alirusha guruneti hilo, lakini mara nyingi serikali imekuwa ikidai ni magaidi ambao ni wapinzani wa Rais Pierre Nkurunzinza.
Takriban watu 700 wameuwawa na wengine laki nne kuikimbia nchi hiyo kufuatia mapigano kati wafuasia wa Rais Nkurunziza na wapinzani tangu April 2015, baada ya kiongozi huyo kutangaza azma yake ya kuwania muhula wa tatu kinyume na Katiba.



