Sunday , 24th Apr , 2016

Ugonjwa wa mnyauko umevamia mashamba ya viazi katika kijiji cha Idimi kata ya Ihango wilayani Mbeya na kuleta hofu ya kuporomoka kwa uchumi kwa wakulima wa zao hilo kutokana na hasara inayotokana na ugonjwa huo.

Wataalam wakiwa katika utafiti wa mbegu za viazi

Hasara zaidi inahofiwa kusababishwa na ugonjwa wa mnyauko kutokana na ugonjwa huo kutajwa kuwa miongoni mwa magonjwa ya mazao yasiyo na dawa, hivyo ni dhahiri kuwa mimea ya mashamba yaliyokwisha athirika haiwezi kupatiwa tiba.

Baadhi ya wakulima wamesema ugonjwa huo haukuwahi kutokea na wameshangazwa kuuona katika siku za hivi karibuni huku wakisema wamejaribu kuwafuata wataalamu lakini wakawaambia ugonjwa huo hauna tiba.

Akizungumzia ugonjwa huo, Afisa ugani wa kijiji cha Idimi Bibi Fromena Komba anasema njia pekee ya kukabiliana na ugonjwa huo ni mkulima kubadili mazao katika shamba husika kila baada ya msimu mmoja.

Bibi Komba amesema sambamba na kubadili mazao kwenye shamba husika inabidi mkulima kuzingatia matumizi ya mbegu bora na zilizoandaliwa kwa umakini badala ya kuokoteza mbegu na kusababisha kutumia hata zile zisizo faa na zilizo na athari kama viini vya magonjwa kama huo.

Wakulima
INAFISA UGANI-FROMENA KOMBA