Saturday , 25th Oct , 2014

Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa manispaa ya Singida wameingiwa na taharuki na kuanza kukimbia ovyo baada fisi kuonekakana katikati ya mji wa Singida akiwa anakimbia na kuingia katika maduka ya wafanya biashara.

Katika hali isiyo ya kawaida wakazi wa manispaa ya Singida wameingiwa na taharuki na kuanza kukimbia ovyo baada fisi kuonekakana katikati ya mji wa Singida akiwa anakimbia na kuingia katika maduka ya wafanya biashara.

Wakieleza kwa hisia tofauti baadhi ya wakazi huku wengine wakiwa wamepanda juu ya mapaa ya nyumba pamoja na watoto wao kwa hofu ya kuumwa,wamesema kuonekana kwa fisi mjini katikati ni jambo la ajabu kwani wanyama kama hao huonekana vijijini au porini, wengine wamesema labda myama huyo amechelewa kurudi vichakani wakati alipokuwa amekuja kula mabaki ya chakula mjini.

Akielezea tukio hilo afisa maliasili mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua amesema pamoja na kwamba wanyama kama fisi wapo katika manispaa ya Singida na pindi wanapo onekana katika maeneo ambayo siyo ya kawaida, wananchi watoe taarifa kwa mamlaka husika kwani wanyama kama hao wanaweza kuwa na ugonjwa wa kichaa, badala ya kujichukulia hatua mkononi ya kuwauwa.

Kutokana na umati wa wananchi kuwa wengi wakati wakimfukuza fisi huyo bila kujali askari waliokuwa wakituliza fujo huku wakiwa na silaha,wananchi walifanikiwa kuwapokonya askari fisi baada ya kumtega na kamba huku wakiimba tunataka fisi wetu na kuamua kumkimbiza mjini huku wakimpiga umbali wa kilomita mbili.