Wednesday , 11th Jun , 2014

Jeshi la polisi limewataka Watanzania kuwafichua watu wanaodhaniwa kuwa na mali walizopata kwa njia ya udanganyifu ikiwemo fedha za wizi wa kughushi, kutokana na wengi kubaki maskini, huku wachache wakinufaika kwa mabilioni ya fedha isivyo halali.

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Tanzania IGP Ernest Mangu.

Mkuu wa operesheni maalum wa jeshi la polisi, Simon Sirro, amesema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari na kuongeza kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kukabiliana na wizi huo kwani taarifa zao zitasaidia mamlaka mbalimbali za kisheria kuweza kuwachunguza watu hao, na kuwafikisha mahakamani.

Amesema nchi imeendelea kuwa masikini kutokana na baadhi ya wajanja kujinufaisha wao na familia zao kwa fedha za wizi, huku wakiacha watanzania wengi wakihangaika na hata kukosa huduma muhimu kama za afya, elimu na huduma nyingine muhimu za kijamii.