Wanafamilia hao wameeleza wao ni wamiliki halali wa nyumba hiyo huku wakionesha hati za umiliki wa nyumba ambapo wameeleza kushangazwa na dalali wa mahakama ya ardhi kuwaondoa kwa nguvu kwa madai ni agizo la mahakama na walipo fuatilia mahakamani walielezwa jalada linalohusu mgogoro wa nyumba hiyo limepotea.
Naye mwenyekiti wa mtaa Juma Hamsini Omari Bashir na majirani wa wanafamilia hao wameeleza kushangazwa na hatua ya mfilisi kuwatoa kwa nguvu katika nyumba yao na kuiomba serikali kuwasaidia kwa kuwa wanawatambua na wanatambua kuwa familia hiyo ni wamiliki halali wa nyumba hiyo.
EATV imemtafuta anayedaiwa kununua nyumba hiyo Josiah Masini mkazi wa morogoro ili kuzungumzia mgogoro huo bila mafanikio.