Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

#FAHAMU Baba wa Tupac alivyokuja kuishi Tanzania

Thursday , 24th May , 2018

Anaitwa Geronimo Pratt ambaye ni baba wa kiroho wa msanii nguli wa hip hop duniani, 2Pac Shakur, na pia ni member wa juu wa Black Panther nchini Marekani.

Pratt alizaliwa tarehe 13 Septemba, 1947, tarehe ambayo mtoto wake Tupac Shakur alifariki katika hospitali ya Las Vegas baada ya kupigwa risasi.

Brad alikuwa mtu wa karibu sana wa mama yake 2Pac Shakur, Afeni Shakur na aliyekuwa mume wake, Mutulu Shakur. (Mutulu Shakur ni baba wa kambo wa 2Pac ambaye ndiye alimlea)

Prat aliingia jeshini na alikuwa miongoni mwa askari waliopigana vita ya Marekani na Vietnam, mara baada ya kutoka jeshini alichukua masomo ya Sayansi ya siasa, na hatimaye kujiunga na Black pather, kundi ambalo liliundwa na Wamarekani Weusi kwa ajili ya kujitetea haki zao, na kufanikiwa kupewa uongozi wa juu kwenye kundi hilo ambalo lilitikisa Marekani.

Mwaka 1968 Geronimo alienda jela kwa tuhuma za kumuua mwanamke mmoja ambaye alikuwa mwalimu wa shule akiwa supermarket na mume wake, ambaye alijeruhiwa, na kumtaja Geronimo ndiye aliyefanya mauaji hayo.

Wakili wa Geronimo alijaribu kumtetea mteja wake kwa kusema kuwa siku ya tukio mteja wake hakuwa eneo la tukio, na alikuwa umbali wa mile 350, hivyo hakuhusika na mauaji hayo, lakini mahakama ilimkuta na hatia na kumuhukumu kwenda jela.

Akiwa jela aliweza kusoma masomo ya sheria na kuhitimu ili kumpa nguvu ya kujitetea kwenye kesi yake.

Geronimo aliachiwa huru na kufutiwa kesi yake baada ya miaka 27 kukaa jela, mnamo mwaka 1997. Kesi yake ilifutwa baada ya kugundua kuwa shahidi alikuwa ni 'informat' wa FBI, hivyo ikaonekana ni kesi ya kutengenezwa.

Baada ya kuachiwa huru walifungua kesi dhidi ya FBI kwa kumfunga kimakosa, kesi ambayo pia alijaribu kumtetea rafiki yake mkubwa kwenye kundi la Black Panther, Mumia Abu-Jamal. Kina Geronimo walishinda kesi hiyo na kulipwa dola million 2.75 .

Baada ya hapo Geronimo alikuja kuishi Tanzania bila watu kujua historia yake na kwa siri kubwa juu ya utambulisho wake, kwani nchini Marekani aliaminika kuwa miongoni mwa watu hatari. Aliishi Tanzania mkoani Arusha mpaka alipofariki June 2, 2011 , na kuacha familia yake wakiwemo mke na watoto.

 

 

 

Source:  2PacLegacy.net

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali