Friday , 1st Apr , 2016

Mamlaka ya Usimamizi wa huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza kushusha bei za umeme kwa asilimia 2 kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.

Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa huduma ya nishati na maji(EWURA), Felix Ngamlagosi.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo Felix Ngamlagosi amesema kuwa Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe.

Bw, Ngamlagosi amesema kuwa punguzo hilo la leo halitawagusa watumiaji wa umeme wanaotumia kuanzia Unit 1 hadi unit isiyozidi 75 na wataendelea kulipa kwa bei ileile.

Aidha Mkurugenzi huyo ameongeza kuwa wateja wakubwa wa majumbani wao wameondolewa gharama za malipo huduma ya kila mwisho wa mwezi na umeme umeshushwa kwa asilimia 2.

Sauti ya Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa huduma za Nishati na Maji (EWURA).