Tuesday , 31st May , 2016

Muangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania, Judith Sargentini (Mbunge wa Bunge la Ulaya), kutoa ripoti kamili ya ujumbe huo, ikiwa ni pamoja na mapendekezo, kuhusu Uchaguzi Mkuu 25 Oktoba 2015.

Muangalizi Mkuu wa Ujumbe wa Waangalizi wa Uchaguzi wa Umoja wa Ulaya (EU EOM) kwa Tanzania, Judith Sargentini (Mbunge wa Bunge la Ulaya), watakutana na waandishi wa habari kesho kutwa ili kuwasilisha ripoti kamili ya ujumbe huo, ikiwa ni pamoja na mapendekezo, kuhusu Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba 2015.

EU EOM ilikuwepo nchini kati ya tarehe 11 Septemba na 8 Desemba 2015, kufuatia mialiko kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Tume ya Uchaguzi Zanzibar.

Kwa ujumla, ujumbe Ulituma waangalizi 141 nchini kote kutoka nchi zote 28 wanachama wa EU, pamoja na Norway, Uswisi na Canada. Ujumbe ulitathmini ni kwa kiasi gani mchakato wa uchaguzi ulizangatia ahadi za kimataifa na za kikanda za uchaguzi, pamoja na sheria za Tanzania.