
Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya msajili wa vyama vya siasa imesema kuwa siku ya tarehe 24 Juni 2016 ndio itakuwa maalum ya kukutana na wananchi wa makundi mbalimbali ili waweze kufahamu sheria inayoongoza vyama vya siasa nchini Tanzania.
Tanzania hivi sasa inashuhudia ongezeko la vyama vya siasa na migogoro katika vyama mbalimbali vya siasa hivyo itakuwa ni nafasi nzuri kwa wananchi na wanasiasa kujikumbusha masuala mbalimbali yahusuyo vyama vya siasa.
