Sunday , 27th Jul , 2014

Baraza kuu la WaisIlamU nchini Tanzania BAKWATA limesema swala ya Eid El Fitri kitaifa mwaka huu itaswaliwa katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es es salaam kuanzia saa moja asubuhi.

SheIkh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Musa Salum

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, SheIkh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Musa Salum, amesema mara baada ya swala kutafuatiwa na Baraza la Eid jioni ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda.

Aidha Sheikh Alhadi amewataka waisilamu nchini kuhakikisha wanaendelea kutenda mema sio kuacha baada ya kuisha kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, bali hata baada ya mfungo na kwamba mengi waliyoyapata katika mfungo yawe ni muendelezo hata baada ya Ramadhani.