Akizungumza katika mkutano mkuu wa chama hicho jijini Dar es salaam ambao unalenga pia kufanya uchaguzi mkuu wa chama hicho, Bw. Dovutwa amesema kwa sasa serikali inaonekana kushindwa kutatua migogoro ya ardhi na kuwaacha wananchi wakinyang'anywa maeneo yao.
Amesema serikali imekuwa ikivutia uwekezaji hapa nchini huku migogoro inayoendelea kati ya wananchi na wawekezaji ikishindwa kutafutiwa ufumbuzi jambo ambalo amesema likiachwa linaweza kuiweka nchi katika hali mbaya.
Bw. Dovutwa amesema licha ya kuwepo kwa migogoro hiyo kati ya wawekezaji na wananchi lakini pia kumekuwa na migogoro mingine baina ya wafugaji na wakulima hivyo migogoro yote hiyo ina wajibu kwa serikali kuhakikisha inaitafutia ufumbuzi vinginevyo watanzania watakuwa ni wageni katika ardhi yao.