Dkt. Abdallah Possi
Mbunge huyo ambaye pia aalikuwa ni Waziri Osifi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Walemavu, tayari amemuandikia barua Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai kuhusu kujiuzulu kwake, na tayari taarifa imeshatumwa kwa Rais.
Kwa upande wake Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Job Ndugai amethibitish taarifa hiyo na kusema kuwa jana (20 Januari, 2017) alipokea barua hiyo ya Dkt. Possi ambayo inatokana na kuteuliwa kwake kuwa Balozi.
Taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano cha Bunge, imesema kuwa kufuatia hatua hiyo ya kujiuzulu ubunge ambayo mezingatia masharti ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 ibara ya 67 (2) (g), ikisomwa pamoja ibara ya 149 (1) (d), Spika wa Ndugai amemuandikia Rais kuwa hivi sasa wabunge wa kuteuliwa na Rais waliopo Bungeni ni saba (7) na hivyo nafasi zilizo wazi ni tatu pekee baada ya Possi kujiuzulu.
Dkt. Possi akiwa Bungeni
Mapema wiki hii, Rais Magufuli aliwateua Abdallah Bulembo na Prof Paramagamba Kabudi kuwa wabunge, na kufikisha idadi ya wabunge 8 ikiwemo wanaume sita na wanawake wawili, hali iliyozusha mjadala kuhusu nafasi tano za wabunge wanawake kwa mujibu kifungu cha 66(1)(e), kabla ya Rais Magufuli kumteua Dkt Possi kuwa Balozi, na sasa Dkt Possi amejiuzulu ubunge na kufanya wabunge wa kiume walioteuliwa an Rais hadi sasa kuwa ni watano.
Kwa mujibu wa kifungu hicho cha Katiba, nafasi tatu zilizobaki Rais atalazimika kuteua wabunge wanawake wote kujaza nafasi hizo