Friday , 1st Jan , 2016

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewaapisha Makatibu wakuu na Manaibu Katibu wakuu wa wizara mbalimbali na kuwasainisha kiapo cha utii na uaminifu leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza mara baada ya kusomewa hati ya utii mbele ya kamishna wa tume ya maadili Rais Dkt. Magufuli aliwataka makatibu wakuu na manaibu hao kama kuna ambaye hajaridhia masharti ya kiapo hicho basi akae pembeni.

Kwa upande wake Waziri Mkuu wa Tanzania amewataka Makatibu wakuu hao wajue kiapo hicho kinamaanisha wameridhia jukumu la kuwatumikia wananchi katika maendeleo huku akisema kuwa utaratibu huo wa kula kiapo cha utii utaendelea kwa viongozi wengine wateule wakiwemo wakuu wa mikoa na wilaya.

Mh. Majaliwa ameongeza kuwa mipango yote ya maendeleo inaanzia kwa makatibu wakuu ambao wana jukumu la kuhakikisha maendeleo yanawafikia wananchi huku wakipata usimamizi wa wakuu wa wilaya na mikoa.

Msikilize zaidi hapa:-

Sauti ya Kassim Majaliwa, Waziri Mkuu wa Tanzania akitoa neno kwa makatibu wakuu baada ya kiapo