Tuesday , 22nd Dec , 2015

Rais wa Jamahuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli amemuhakikishia mwakilishi makazi wa banki ya Maendeleo ya Africa Dkt. Tonia Kandiero kuwa serikali yake itaendelea kushirikiana na benki hiyo katika utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli alipokutana na Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt. Tonia Kandiero

Rais Magufuli ameyasema hayo jana baada ya kutembelewa na mwakilishi mkazi wa banki hiyo Ikulu jijini Dar es Salaam ambapo amesema kuwa serikali yake itahakikisha maendeleo yanakuja kwa haraka kupitia beki hiyo.

Pamoja na kumhakikishia ushirikiano huo Rais Dkt. Magufuli ametoa wito kwa benki hiyo kupunguza michakato ya kuelekea katika utekelezaji wa miradi na badala yake uwepo utaratibu wa haraka katika kutekeleza miradi hiyo katika kipindi kifupi.

Aidha rais magufuli pia amekutana na balozi wa Rwanda hapa nchini Mh. Eugine Kaihura Ikulu Jijini Dar es Salaam huku akimpa salamu kutoka kwa raisi kagame kufurahishwa na hatua ambazo amechukua hata katika usimamizi na utendaji kazi wa Bandari.

Aidha balozi Eugine amuhakikishia kuwa Serikali ya Rwanda iko tayari kushirikiana na Tanzania hasa kuitumia bandari ya Dar es Salaam ambayo hupitisha zaidi ya asilimia 70 ya mizigo ya Rwanda.