Friday , 26th Dec , 2014

Makamu wa Rais Dk Mohammed Gharibu Bilal amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutowaficha majumbani watoto wanaobainika kuwa na matatizo ya moyo

Dkt Bilal amewataka wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kutowaficha majumbani watoto wanaobainika kuwa na matatizo ya moyo kwa kisingizio chochote na badala yake wawapeleke katika vituo vya kutolea huduma ili waweze kupatiwa matibabu mapema.

Dkt. Bilal amesema hayo jijini Dar es saalam wakati akiwaaga watoto 55 wenye matatizo ya moyo wanapelekwa nchini India kwa matibabu na kubainisha kuwa serikali inaendelea kufanya kila linalowezekana ili kuhakikisha inapunguza vifo vitokanavyo na matatizo hayo.

Kwa upande wao wazazi na walezi wa watoto wanaopelekwa nchini India mbali na kutoa shukrani zao kwa wafadhili wa safari hiyo wametoa wito kwa wadau wengine kuendelea kuongeza nguvu ili kuwasaidia watoto wengi zaidi.

Baadhi ya wahisani waliofanikisha safari hiyo wamesema wataendelea kupambana na tatizo hilo linaloendelea kuongezeka mwaka hadi mwaka na kutoa wito kwa wadau wengine kuendelea kujitolea.